Kepteni Temba, Mkurugenzi wa Fungakazi Modern Taarabu. |
Baada ya wimbo kupotelea kusikujulikana Temba hakuishia hapo alihama studio na kwenda kurekodi kwa mara ya pili katika Studio ya Soundcrafters Temeke.
Sasa sekeseke likaanza baada tu ya kutoka kwa wimbo huo studio na kuanza kusikika redioni. Mkurugenzi wa Funga Kazi Modern Taarabu bwana Kapteni Temba amekuwa akipata sms za vitisho na watu wasiojulikana wakimtumia sms katika simu yake jambo lililomlazimu kubadili line ya simu yake.
Watu hao waliendelea kuwatumia sms hata watangazaji ambao wamekuwa wakiupiga wimbo huo au wameonekana kama kushabikia kwa namna moja ama nyingine na wao wamekuwa wakitumiwa sms za vitisho wakiambiwa waache kucheza wimbo huo.
Pia baadhi ya wadau wa taarabu nao wamekuwa wakitumiwa sms hizo za vitisho toka kwa mtu asiejulikana wakiaswa kuacha kushabikia mambo yasiyowahusu.
Kepteni Temba baada ya kuona hali inaendelea vile akaamua kwenda kuripoti polisi vitisho hivyo.
1 comments:
Mungu atawashinda na shari zao..funga kazi level nyengine wasokubali wajinyonge kwa big G.
Post a Comment