Tokea kifo cha wasanii 13 wa 5 Star mpaka sasa ni wengi
wametangulia mbele ya haki tukiamua kuwataja mmoja mmoja, lakini swali
linakuja nini wamefanya hata tu kuwaenzi wasanii waliofariki hata
kufanya kisomo cha pamoja kuwarehemu tu!.
Mimi kama mwandishi wa taarabuzetu.blogspot.com na mdau mkubwa wa mziki huu wa mwambao, Katika kumbukumbu zangu 5 Star
walifanya hitma ya pamoja iliyofanyika katika ukumbi wa PTA mtoni kwa azizi
ally lakini baada hapo hakuna kilicho endelea tena, wakati mwingine
huwa napatwa na maswali kwani katika tasnia ya taarabu hakuna chama
kinachotetea masirahi na haki za wasanii? na kama kipo kinafanya kazi
gani? ni aibu sana.
Viongozi wa Bendi za Taarabu ni vyema kama mngekaa pamoja mkajipanga kama timu moja mkaelewana namna ya kuweza kundeleza bendi pamoja na mambo mengine ya muhimu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Hili ni la msingi sana na nimekua nikilipigia kelele kwa nguvu zangu zote ila watu wa Taarab ubinapsi umezidi sana na majungu na ufahamu finyu ndio tatizo
Siku zote umoja huwa muhimu sana, sasa hawa watu wa Taarabu wao wanajiona akiwa peke ya ni vizuri zaidi na akimshirikisha mwenzake anaona kama atakuwa amemtoa, yaani kifupi ni Ubinafsi na Majungu mengi.
Kamwe haitatokea wameungana...
Post a Comment