TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, October 26, 2016

YAH TMK TAARAB - YAIBOMOA JAHAZI MODERN TAARAB...



NI BENDI YAH TMK TAARAB -  YAIBOMOA JAHAZI MODERN TAARAB, YACHUKUWA SILAHA MUHIMU ZA KAZI.

Ule usemi unaosemwa na baadhi ya wadau wa taarab ya kuwa "Jahazi Modern Taarab bila ya Mzee Yussuf linasuasua" unaonekana kama unakubalika kwa asilimia fulani baada ya bendi hiyo kupoteza waimbaji muhimu pamoja na wapiga vinanda. 

Majina ya Fatma Nyoro, Chidi Boy, Moh'd Mauji, Mussa Mipango, Kichupa kwa sasa hayatosikika kwenye maonesho ya Jahazi. 

Pia kuna tetesi kuwa Khadija Yussuf ameenda Wakaliwao kwa Thabit Abdul.

Bendi ya TMK pia imeibomoa Coast Modern Taarab kwa kumpa shavu Omary Teggo na dada yake. 
Pia Bi Mwanahawa Ali (JEMBE GUMU) ametilishiwa saini katika bendi hiyo huku akipewa wimbo wa "SINA PUPA MUNGU ATANIPA".

#HAYA SASA - HAPA KAZI TU...


0 comments:

Post a Comment