TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Friday, August 2, 2013

DOWNLOAD:- Nyimbo mpya kabisa ya Mashauzi Classic - BONGE LA BWANA...


Nyimbo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa Taarabu nchini “BONGE LA BWANA” sasa ipo hewani.

BONGE LA BWANA imerekodiwa katika Studio za Soundcrafters kwa Enrico.
Kinanda kimepigwa na Kally akishirikiana na Thabit Abdul.
Solo limepigwa na Ramadhan Kisolo.
Bass amepiga Jumanne Boya, Johncena Bass.

Akizungumza na mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com mwimbaji wa wimbo huo Hasheem Saidy(Mzee wa Majanga) alisema:- “Mzigo wenyewe ndo huo hapo nimeuachia watu wausikilize, naamini wataupenda tu na asiyeupenda aseme...”, alisema na kuongeza “Maana mashairi yametulia na yanamvuto wa hali ya juu, vyombo vimepigwa na wataaramu tupu, mi nasema mwaka huu ni wetu hakuna atakayetukamata na katika show zetu tunataka kuwaonesha kuwa Mashauzi Classic ipo juu!!”.
Mashauzi Classic Modern wakiwa mzigoni...
Katika msimu huu wa sikukuu za Idd Mashauzi Classic watakuwa Mji kasolo Bahari siku ya IDD Mosi, na Show zingine watakuwa Mbeya na Songea, katika show zote watapiga nyimbo mpya na nyimbo zote zinazotengeneza Albam yao mpya pamoja na nyimbo za zamani watazikumbushia pia.

BONGE LA BWANA Inakamilisha Albam ya Tau “3” ya Mashauzi Classic, Albam imebeba jumla ya nyimbo Sita “6”.
Nyimbo zilizomo katika Albam hiyo pamoja na waimbaji ni kama ifuatavyo:-
1.  “Asiekujua hakuthamini”, umeimbwa na Isha Mashauzi na Saida, “Wimbo huu ndo umebeba jina la Albam”.
2. “Ni mapenzi tu”, umeimbwa na Zubeda Malik,
3 . “Ropokeni yanayowahusu”, umeimbwa na Saida Ramadhan.
4. “Mapenzi hayana dhamana”, huu umeimbwa tena na Isha Mashauzi,
5. “Tupendane”, umeimbwa na Saida Ramadhan.
6. “Bonge la Bwana”, Umeimbwa na Hasheem Saidy
Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi...!!!
Hii ndo Albam yenye nyimbo Sita kali kabisa toka kwa Mashauzi Classic Modern Taarabu.
Mtandao huu ulipoulizia siku ya Uzinduzi alisema muda bado haujapangwa hivyo tutawataarifu, tunajipanga kwa kuja kutoa burudani kali zaidi siku ya Ufunguzi…!!

2 comments:

Anonymous said...

GOOD WORK MDADA....

Unknown said...
This comment has been removed by the author.

Post a Comment