TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, August 6, 2013

ISHA MASHAUZI NA HEMEDY OMARY, WAJA NA "MASIMANGO HAYAFAI"...

 
Isha Ramadhan wa Mkurugenzi wa Mashauzi Classic na Hemed Omary wa T.O.T.

Isha Ramadhan (Mashauzi) na Hemedi Omary kwa pamoja wanakuja na wimbo wakushirikiana uitwao "Masimango hayafai". 

Akizungumza na mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com Hemedi Omary alisema kwamba wimbo huo ni maandalizi ya albam yake binafsi nje ya bendi yake ya TOT na itaitwa hivyo hivyo "Masimango hayafai". 

Hemedi alizitaja nyimbo nyingine kuwa ni "mwaka huu nimefika", "Silumbani na wakuja" na "huna ujanja" itakayoimbwa na Mwasiti Suleiman. 
Wimbo wa "Silumbani na wakuja" utaimbwa na Isha Mashauzi peke yake. 

Aliongeza kwa kusema wadau wajiandae kupata kitu kizuri kabisa nakiandaa.

0 comments:

Post a Comment