TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Saturday, August 10, 2013

BI MWANAHAWA ALLY AWAPIGA CHENGA 5 STAR'S NA G5 NA KUIBUKIA EAST AFRICAN MELODY...!!

Mkongwe katika Taarabu Bi Mwanahawa Ally (Jembe Gumu).
 Kama ambavyo mwenyewe amekuwa akijiita "Jembe Gumu" Bi Mwanahawa Ally ameushangaza umma wa wapenda taarabu nchini Tanzania baada ya kuonekana katika jukwaa la East African Melody pale buguruni siku ya jana kwenye IDDI MOSI. 

Mwana hawa alionekana katika jukwaa moja na waimbaji wa kundi la East African Modern Taarabu badala ya kuwa katika bendi yake ya 5Stars Modern Taarabu.

Mwandishi wa habari hizi alipomhoji imekuwaje anaonekana East african melody? wakati ana mkataba wa miaka miwili na 5Stars!? alijibu ya kwamba yeye si msanii wa 5Stars kama inavyosemekana! kwani wenyewe 5Stars wamekiuka mkataba mpaka sasa, "hawajanimalizia pesa yangu ya mkataba hivyo nimejiondoa na kama wanataka niwalipe pesa zao waseme wanataka niwalipe kwa style ipi, sababu pia tayari nimetumikia sehemu ya mkataba wao! nimesikia maneno ya watu kwamba hao viongozi wa 5Stars wanataka kunikamata na kunishusha stejini siku nitakayoonekana naimbia bendi nyingine.. nawaambia hawawezi na kama kweli wanaweza waje leo hapa Buguruni kunikamata tuone! Mimi mwenyewe nina haki ya kuwashitaki sababu wamekiuka mkataba tuliowekeana" Alipoulizwa vipi kuhusu G5 nayo? 
 
akajibu "Pale nimeimba wimbo mmoja tu na wala sina mkataba nao kifupi wale nawaona kama wanangu sina tatizo nao". 

Mkurugenzi wa 5Stars hakupatikana kwenye simu yake ili kuweza kuthibitisha haya, taarabuzetu.blogspot.com inaendelea kufuatilia ishu hii ili kujua nini ukweli hasa!.

0 comments:

Post a Comment