TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, August 4, 2013

MRISHO RAJABU (B.S.S.):- VIDEO YA "CHANGA LA MACHO" ITAKUJA KUWASHIKA...

Mrisho Rajabu (BSS)
 Rais wa Bendi ya King's Modern Taarabu Mrisho Rajabu "B.S.S." Amejitamba kwamba video yake aliyoifanya katika bendi hiyo ina ubora mkubwa sana.

Rajabu amezungumza na taarabuzetu.blogspot.com na kusema video hiyo ameifanyia mkoani mbeya ili kuleta radha tofauti za mazingira na si kama video zingine za taarabu zinavyofanana location. "Ndugu mwandishi video ya changa la macho imegharimu kiasi kikubwa cha pesa hivyo mashabiki zangu wategemee kitu kizuri nasisitiza tena". 

Kings Modern Taarabu mwezi uliopita walikuwa na ziara ndefu sana takribani wiki mbili katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Mbeya. Sumbawanga na Mpanda.

0 comments:

Post a Comment