TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Thursday, August 8, 2013

FITINA MPOGO WA 5 STAR'S MODERN TAARAB, APANIA KUWAKALISHA WAKONGWE!!...

Fitina Mpogo.
Muimbaji chipukizi mwenye haiba ya kike haswa Fitina Mpogo ameuambia mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com Kwamba ameamua kuja kivingine kabisa safari hii,
"kwani najua wazi kwamba muziki ni kazi yangu kwahiyo nina kila haja ya kujituma na kumshawishi director wangu Thabit abdul kuniamini na kunipa nyimbo". Fitina alisema kwa kujiamini

Mwandishi wa habari hizi aliona isiwe tabu akampigia simu Director Thabit ili kutaka kujua uwezo wa Fitina Mpogo ndani ya 5 stars. Thabit alisema Fitina ni muimbaji anaejituma sana na anajiamini, pia ana sauti nzuri ya kuimba, ki-ukweli anaweza, mimi kama Director naweza kumfikiria kwa hilo maana uwezo wake unaonekana na ameonesha nia ya kweli. Wakongwe katika game wajiandae.

0 comments:

Post a Comment