TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, August 4, 2013

HII NI TANO BORA (5) YA WAPIGA VINANDA KATIKA TAARABU NCHINI TANZANIA 2008 - 2013!!...

Kinanda ni chombo muhimu sana katika muziki wa Taarabu, Kumekuwa na wapigaji wengi sana wa vinanda karibu kila bendi. lakini ifuatayo ni orodha ya wapigaji watano bora wa vinanda. ikumbukwe hii ni kwa mujibu wa mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com na wala si-vinginevyo!!. 

1.= Thabit Abdul:- Inawezekana ni sababu amepiga miziki aina tofauti, kwani amekuwa akifanya vizuri sana katika nyimbo tofauti. Thabit kwa sasa ndio mtu anae ongoza kwa kufanya kazi na waimbaji tofauti wa Taarabu na kuwatengenezea nyimbo zao. 
Thabit Abdul kwa sasa ni Director wa 5 Stars na albam ya sasa ya 5 Stars katunga yeye nyimbo zote na kupiga kinanda pia. 

2.= Ally J:- Yeye anakamata nafasi ya pili kwa upigaji wa kinanda, ni Director anaekubalika sana katika tasnia hii hususani Modern Taarabu. Ally J ambae pia hivi karibuni amejiingiza kwenye uimbaji na wimbo wake wa "Ukurasa mpya" unafanya vizuri sana katika vituo mbalimbali vya redio. Ni miongoni mwa wasaani waanzilishi wa 5 Stars pia. 

3.= Chidy Boy:- Tegemeo kubwa la Mzee Yusuph kwa sasa pale Jahazi. wakati anaingia Jahazi wengi walimbeza na kumuona hafai lakini kadri siku zilivyokuwa zinakwenda alionyesha ushupavu mpaka kufikia Mzee Yusuph kumuamini na kumpa nyimbo muhimu kabisa za bendi kupiga yeye. kwa sasa ndio mpiga kinanda namba moja pale Jahazi Modern Taarabu. 

4.= Omary Kisila:- Wasiomjua huwa wanafikiri Omary Kisila kaibuka tu katika wimbo wa Domo la udaku!, lah! hasha! Kisila ni mkongwe katika muziki wa Taarabu kwani ameshawahi kufanya kazi na mzee yusuph, Bi Sihaba Juma, Zuhura Shabban na wengineo pale Zanzibar Stars, kwa sasa ni mpiga kinanda namba moja wa T MOTTO chini ya mkurugenzi Amin Salmin "komandoo". 

5.= Ndage Ndage:- Alianza kupiga kinanda akiwa na umri mdogo kabisa, tena anatoroka shule na kwenda kwa kaka yake Ally J kufundishwa kinanda. hivi sasa Ndage Ndage amekuwa mwalimu na yeye anawafundisha wengine. Kwa sasa yupo katika bendi ya Mashauzi, ila kuna muda alienda Kings modern taarabu kwa muda mchache lakini akarejea Mashauzi Classic ambapo ameendelea kuwepo mpaka sasa. Huyo ndio Ndage Ndage midole ya tembo a.k.a. mtoto wa Thabit abdul.

4 comments:

Unknown said...

Mmmmmh.... mbona mfalme mzee yusuph hayupo humu ndani????????

Anonymous said...

Kwel kabisa me mwnyw nljua mzee atakuepo lakin cvyo.penye cfa achen pasifiwe ata km unasema kwa mujibu wa blog hii.me naona mfalme alistahli kabisa tena namba1.cjasema km hao hawastahl ila mzee anaweza kiukwel.lilian masika mdau no1

Anonymous said...

yaa mzee amgekuwepo lkn hamfikii Thabit wala ally j!labda angakaa namba tatu,moja na mbili no!hao watu wakali sn!

Anonymous said...

Ushaambiwa mfalme ye kawaachia wadogo zake

Post a Comment