TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, August 4, 2013

MKURUGENZI WA G5 MODERN TAARABU HAMISI SLIM, AAHIDI MAKUBWA KWA WAPENZI WA BENDI YAKE..

Mkurugenzi wa G5 Modern Mr. Hamis Slim
 Hamisi Slim ni jina kubwa sana hususani katika tasnia hii ya Taarabu nchini Tanzania, Hapo kabla alishawahi kuongoza bendi ya 5 Stars kabla haijapata ajali, Ila kwa sasa ana miliki bendi yake mwenyewe iitwayo G5 Modern Taarabu yenye makazi yake Mtoni kwa Azizi Ally Dar. 

Akizungumza na Taarabuzetu.blogspot.com Slim alisema kwa sasa bendi yake ipo jikoni kwa maandalizi ya nyimbo 4 kali.
Mkurugenzi huyo wa G5 Modern aliongeza pia kuwa ana mpango wa kuongeza wasanii wenye majina makubwa toka katika bendi kongwe ambazo hakuzitaja wala majina ya wasanii anaowahitaji, 
Aliongeza, "nipo hatua za mwisho mwisho kumalizana nao, Nimejipanga vyema".

0 comments:

Post a Comment