TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, August 6, 2013

BI MWANAHAWA ALLY, AZICHANGANYA 5 STARS NA G5 MODERN TAARAB...!!.

 
Bi Mwanahawa Ally.

Muimbaji mkongwe wa Taarabu nchini Tanzania Bi Mwanahawa Ally ameendelea kusumbua kama ilivyo kawaida yake lakini muda huu ni 5 Star's na G5 Modern Taarabu. 

Sa sijui atajigawa vipi katika show, Ukiangalia Posters za 5 Stars na za G5 Modern kwenye shangwe za IDDI kote yupo!, na kuna habari ambazo sio rasmi zinasema kwamba Bi Mwanahawa Ally tayari ametumiwa nauli na G5 toka unguja kuja Dar kwa ajiri ya kuimba katika matamasha ya  sikukuu ya IDDI. 

Ikumbukwe kuwa Bi Mwanahawa Ally tayari ana mkataba wa miaka miwili na 5 Star's Modern Taarabu ambao haujaisha!. 

Taarabuzetu.blogspot.com hakuona shida, ikawapandia hewani viongozi wa 5 Stars, simu iliita na kupokelewa wanasema hawana taarifa nae!.

Ngoja tusubiri...!!

1 comments:

Unknown said...

mama anatafuta magome wamuache kwa speed yake.. kisu kikali ndo kitakacho pata

Post a Comment