TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, August 20, 2013

CHAMA CHA TAARABU TANZANIA, MBONA MPO KIMYA JUU YA MGOGORO WA BI MWANAHAWA NA MMILIKI WA 5 STAR'S...!!?


 Mgogoro wa mwanamuziki mkongwe wa taarabu nchini Bi Mwanahawa Ally na mmiliki wa 5 Star's Modern Taarabu Mr Shark's umeingia sura mpya ya malumbano juu ya mkataba waliowekeana wakati wa kusaini. 


Mtandao huu ulikuwa wa kwanza kabisa kuandika juu ya malalamiko ya Bi Mwanahawa akilalamika kukiukwa baadhi ya vipengele katika mkataba huo, na kuongeza kwamba yeye si msanii tena wa bendi hiyo sababu mmiliki huyo ameshindwa kutimiza masharti ya mkataba. 

Jumapili ya wiki iliyopita nae mr Shark's alisikika katika kituo kimoja cha redio hapa jijini akilalamika kwamba Bi Mwanahawa amekuwa haheshimu mkataba wa miaka miwili aliosaini mwenyewe huku akiwa na akili timamu kabisa, amekuwa akimtia hasara mbalimbali ikiwemo kumlaza hotel kwa siku zote alizokuwa akiishi hapa Dar! na hasara nyingine nyingi sana. 

Blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com kama mdau mkubwa wa muziki huu tumekuwa tukijiuliza maswali kadhaa, hivi chama cha taarabu nchini hakiyasikii malumbano haya?, na kama inasikia ni hatua gani wamechukua katika kutatua tatizo hili kati ya mmiliki wa bendi na msanii?. au hakuna kabisa chama hicho hapa nchini?, haki za msanii wa Taarabu hapa atazipata wapi kama hakuna chama?. 

Kila muziki una chama chake hapa Tanzania lakini katika Taarabu kama chama kipo basi hakina makali na wala hakiwezi kutoa kalipio la aina yoyote wanachama wake ambao ni bendi wakaelewa!, ndio maana hata katika mashindano ya Kilimanjaro Music Awards Taarabu imekuwa haitendewi haki katika kupanga makundi ya wagombea, mfano hakuna wagombea chipukizi, pili kipengele cha mburudishaji bora wamekiondoa na watu wapo kimya tu! 

Wakati umefika kwa viongozi wa mabendi ya Taarabu kuitisha mkutano na kuwaomba Basata kuitisha mkutano wa kuchagua viongozi wakuongoza Chama hicho. 

Na kama kweli chama kipo hai basi waamke sasa katika kutetea haki za wasanii wa taarabu nchini na sio kukaa kimya tu kama ilivyo sasa. 

Hili tatizo la Bi Mwanahawa Ally liwe mfano kwa utendaji bora wa chama hicho, tutoke giza na kuangaza macho!, ndio maana watu binafsi wamekuwa wakifaidika zaidi kwa muziki huu na kuacha msaani ambae ni mvuja jasho akibaki na labda!.

Kalamu naweka chini...kamwe siwezi kuwa adui kwa kusema kweli. TAARABU DAIMA MBELE KURUDI NYUMA MWIKO!!.

0 comments:

Post a Comment