TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Saturday, August 3, 2013

THABIT ABDUL MBUNIFU ALIEITOA TAARABU KWENYE "MODERN" MPAKA "TARADANCE"

Thabit Abdul
KWA SASA!. Muziki wa taarabu umekuwa ukibadilika kila kukicha na hii yote inatokana na teknorojia kuongezeka. 

Mwanzoni ilikuwa Taarabu asilia watu wakaipenda, Katikati ikaja ikawa Modern taarabu watu wakaipenda pia. Lakini kwa sasa ni TARADANCE watu ndio wanaipenda zaidi... Muanzilishi wa mtindo huu wa Taradance ni Thabit Abdul ambae anasema kwa mara ya kwanza aliutumia pale Mashauzi Classic kabla hajahamia 5 Stars. 


Nilimuuliza nini tofauti ya Modern Taarabu na Taradance kiufundi? 
Thabit alijibu kwamba Modern ni style ambayo inatumia vyombo au ala zile zile zilizotokana na taarabu asilia ila kuna vitu fulani watu wameviongeza ili kunogesha zaidi muziki huu Ila mimi nilipoingia katika tasnia hii nikitokea kwenye dance, nikasema ni lazima nifanye kitu cha kuweka historia kwenye muziki huu wa taarabu, maana nimeshapigia Twanga Pepeta, TOT band, Extra Bongo na nyinginezo nyingi, nikaanzisha mtindo nikauita TARADANCE, yaani ni taarabu yenye vionjo vya DANCE ndani yake!. Nikaanza kutumia beat za DANCE katika nyimbo nyingi za Mashauzi Classic na wasanii mmoja mmoja wasio na bendi, mpaka sasa namshukuru mungu imekubalika. Huyo ndio Thabit..

0 comments:

Post a Comment