TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, December 9, 2014

FIVE STARS: JIANDAE KUPATA NYIMBO TATU KALI...!! PATA PICHA ZA STUDIO NA MAJINA YA NYIMBO...

Baadhi ya wasanii wa kundi la 5Stars.

Kundi zima la Taarab 5Stars leo wameingia studio kurekodi nyimbo zao Tatu watakazoziachia hivi karibuni baada ya kumalizika kurokodiwa.
Mmoja wa viongozi wa kundi hilo kongwa ameongea na Taarabuzetu.blogspot.com na kuihakikishia kuwa nyimbo hizo zitakuwa nzuri na itakuwa ndo habari ya mjini zitakapotoka.

Amezitaja nyimbo hizo ni:-
UBAYA HAUNA SOKO - Mwanaidi Ramadhani.
KISHTOBE - Salha wa Hammer Q.
SINA GHUBU - Mape Kibwana.

Wapenzi wote wa Taarabu kaeni mkao wa burudani.
Je! Wajua maana ya "Kishtobe"?????

Zifuatazo ni picha mbalimbali wakiwa studio wakirekodi...

Waimbaji wa 5Stars.

Mape Kibwana, Anaimba "Sina Ghubu".
Mwanaidi Ramadhani akiimba "Ubaya hauna Soko".
Salha wa Hammer Q Akiimba "Kishtobe".
Salha akiwa na Ally J (Boss) ambaye amepiga vinanda ktk nyimbo hizo.

0 comments:

Post a Comment