TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, December 21, 2014

ISHA MASHAUZI KUIKOSA MIAKA 8 YA JAHAZI TRAVERTINE HOTEL LEO USIKU...


Isha Mashauzi.
Mkurugenzi wa Mashauzi Classic Isha Mashauzi ataikosa show ya Jahazi Modern Taarab kutimiza miaka minane tangu izaliwe.

Show hiyo inafanyika leo usiku katika ukumbi wa Travertine Hotel huku ikiaminika kuwa wasanii wote walioitumikia Jahazi watakuwepo.

Katika onyesho la Mashauzi Classic pale Mango Garden Alhamisi iliyopita, Isha alitumia kipaza sauti chake kuinadi show ya Jahazi na kuwataka wapenzi wa Mashauzi wasikose kwenda Travertine Jumapili.

Lakini mashabiki hao walipomuuliza kama na yeye atakuwepo, Isha akawajibu kwa kusema kuwa kwa bahati mbaya yeye hatakuwepo.

“Nina kazi nje ya mji, nasikitika kuwa sitakuwepo katika onyesho hilo, lakini nawatakia mafanikio mema na naomba mkawaunge mkono,” alisema Isha.

0 comments:

Post a Comment