TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Friday, May 1, 2015

Dar Modern Taarab kufanya ziara kubwa mikoani - "MODERNICA NA DAR MODERN".



 Dar modern taarab chini ya uratibu wa on point solutions limited wanatalajia kufanya ziara katika mikoa ya Mbeya, Rukwa, Katavi, Dodoma, Morogoro na Dar
Akiongea na mtandao huu wa taarabuzetu.blogspot.com mratibu wa ziara hiyo Bw Emmanuel Saimon amesema ziara itakayo julikana kwa jina la MODENICA NA DAR MODERN itaanzia mkoani Mbeya katika wilaya ya Kyela katika mji wa Kasumulo mpakani mwa Malawi na Tanzania siku ya j5 tar 20/05 kwenye ukumbi wa White ston.

Amesema baada ya hapo itafatiwa na show ya pili Mpanda ijumaa tar 22/05 ktk ukumbi wa Ruju social hall.
Show ya tatu itakua siku ya jmosi tar 23/05 Rukwa ktk mji wa Sumbawanga ktk ukumbi wa Upend hall.

 Mratibu wa ziara hiyo amesema baada ya show hizo watarejea jijini Dar kwa onyesho la ijumaa tar 29/05 ndani ya uwanja wa taifa wa taarab Travertine Hotel Magomen.

Jumamosi tar 30/05 wataelekea Dodoma katika ukumbi wa Royal village na kumalizia ziara hiyo mjini Morogoro katika wilaya ya Kilosa kwenye ukumbi wa Babylon.
Uongozi wa on point solutions na Dar modern umewaomba wapenzi na mashabiki wa taarab wa sehemu husika kujitokeza kwa wingi kuja “Kumodenika na dar modern taarab” kwani wamewaandalia mambo mazuri.



* Picha zote zilichukuliwa siku ya Jumatano ya tarehe 29/05/2015 Asubuhi katika ukumbi wa Habari Maelezo IPS Posta siku hiyo kulikuwa na mkutano na waandishi wa Habari ambapo Mkurugenzi wa On Point Solutions Ltd Bw Bahati Singhaliongelea juu ya ujio mpya wa Dar Modern na mtindo wao mpya wa "Modernica na Dar Modern".

0 comments:

Post a Comment