TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Friday, July 3, 2015

Hamis Slim wa G5 Modern Taarab atangaza nia...!!!

Mkurugenzi wa G5 Modern Taarab Mr. Hamis Slim
Mkurugenzi wa bendi ya Taarab ya G5 Modern Taarab Mr. Hamis Slim, ametangaza rasmi nia yake ya kuwatumikia wananchi wa Mtoni kwa Azizi Ally.

Hamis alijieleza mwenyewe katika maelezo haya hapa:-

Assalaam aleyko watanzania wenzangu hususani wanamtoni wenzangu, tumshukuru mungu kwa kutufikisha tena salama ktk mwezi huu mtukufu wa ramadhani mwezi ambao unatufanya tumrudie mola wetu kwa kutimiza zile nguzo tano za kiislam.

Pamoja na hayo pia mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi basi itakuwa si vibaya mimi km kijana imara niliyelelewa madhubuti na Chama Cha Mapinduzi kutangaza nia yangu ya kutaka kugombea nafasi ya Udiwani ktk kata yangu ya Mtoni.

Mimi kijana mwenzenu Hamis Slim wakati ukifika nitachukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ya udiwani wa kata ya Mtoni kwa minajali ya kuleta maendeleo muonekano na si maendeleo simulizi, shime vijana wenzangu tuamke sasa tuungane mkono kulikomboa taifa letu kwa mawazo chanya kwa pamoja tunaweza.

Nitaomba nafasi baada ya kutafakari takribani miaka mitano na kuona fursa nyingi tulizonazo ktk kata ya Mtoni kushindwa kutumiwa kwa maslahi na manufaa ya wananchi wa mtoni
Badala yake kutumiwa na watu wengine wa nje ya mtoni.

Changamoto hizi ndizo zilizonilpelekea kuwa na maamuzi ya kugombea kwa ajili ya kuleta Mabadiliko mapya, Fikra mpya, Ubunifu mpya, Uongozi mpya na kuondoa uongozi ulio na mawazo mgando.

Kwakuwa uwezo ninao sababu ninazo nia ya kugombea ninayo kwa pamoja na wanamtoni wenzangu tutashinda na kuibadili na kuivusha kata ya mtoni pale ilipofikishwa hakika SLIM ndio chaguo lako (HAMIS SLIM HAKIKA ATATUFIKISHA)
Bwana Hamis alipoulizwa kuhusu kugombea Ubunge alisema:-

Naamini kila mtu anatamani kugombea nafasi hiyo ya Ubunge, ni nafsi kubwa sana ambayo nitafanya hivyo baada ya kuwatumikia kwanza wananchi wenzangu na kuona uwezo wangu katika utendaji kazi, nataka wananchi wenyewe waje kusema kama nafaa. Najiamini ipo siku nitakuwa pale Bungeni kutetea na kuleta maendeleo ya wananchi wangu, watanzania wenzangu.

Taarabuzetu.blogspot.com inakutakia kila la kheri Bwan Hamis Slim.


0 comments:

Post a Comment