TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, July 9, 2014

Mashauzi Classic: Mmoja aachishwa kazi na mwingine asimamishwa...


Mkurugenzi wa Mashauzi Classic - Isha Mashauzi.
Kundi la Taarab Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi linalofanya shughuli zako jijini Dar es Salaam, Tanzani na Show zake kila Alhamisi hufanyika Mango Garden imewasimamisha kazi wasanii wake wawili.

Taarifa zilizofika katika meza yetu ya Taarabuzetu.blogspot.com zinasema wasanii hao wamesimamishwa toka Ijumaa ya tarehe 13/06/2014, waliosimamishwa ni Thania Msomali na Fatma Seif.
Fatma Seif katika kundi hilo la Mashauzi amewahi kuimba nyimbo iitwayo “Mdomo wako utakuponza” katika albam ya “Si bure unamapunngufu”.
Habari zilizotufikia kwa upande wa Fatma kisa cha kusimamishwa ni kutohudhuria show ya Mashauzi siku hiyo na kudaiwa kuonekana katika bendi ya Gusagusa Min iliyokuwa na Show pia siku hiyo.
Mwandishi wa habari hii baada ya kupata habari hizi alimpigia simu Fatma mwenyewe aweze kueleza kisa hasa cha yeye kusimamishwa kazi.
Fatma:- “Mimi siku hiyo sikwenda kazini kwasababu nilikuwa naumwa, kiongozi wangu alinipigia simu kuniambia nihudhulie kwenye show nikamwambia siwezi kwasababu naumwa, akaniacha siku ya pili yake akanipigia simu tena kuniulizia hali yangu nikamwambia bado nipo nyimbani tu, lakini cha kushangaza akanitumia ujumbe kuwa kunisimamishwa kazi miezi mitatu (3), kesho yake akanitumia ujumbe tena wa kuwa Nimeachishwa kabisa kazi hivyo niko huru kutafuta bendi yoyote, kwakweli imeniuma sana maana sijui kama ndo hili tatizo la mimi kuugua.
Alipoulizwa Fatma amechukua uamuzi gani?
"Sijachukua uamuzi wowote na hivi sasa nipo tu nyumbani bado akili yangu haijatulia hivyo sijajua kitu cha kufanya, acha kwanza nitulie".

KWA UPANDE WA THANIA MSOMALI:
Baada ya kuhojiwa na mwandishi wa habari hii alisema:
Thania:- “Mimi nilikuwa naumwa na nilitoa taarifa kwa uongozi, nimeenda Hospitali kufanyiwa uchunguzi nikaonekana (Akataja ugonjwa) hivyo nikaandikiwa dawa ambazo niliendelea kuzitumia, baada ya kama week mbili nikawa najisikia vizuri na nikaamua kwenda kuripoti kazini lakini cha kushangaza kidogo nikaambiwa niendelee kupumzika kwanza mpaka nipone ndo niende, nimekaa nyumbani tena baada ya siku kadhaa Mashauzi walikuwa wanapiga Mango nikaomba tena nihudhulie kazini ila nikaambia nisubiri tu ila nikaomba basi niende kuangalia show nikaruhusiwa ila sikuimba.
Sasa kinachoniweka njia panda ni kuwa, hali yangu ni nzuri nimeimarika ki-afya na ninahamu ya kuimba ila nikiuelezea uongozi wangu kuwa nataka kuripoti kazini wanasema nisubiri tu sasa nitasubiri hadi lini!? Kwa kweli sijajua muafaka upo wapi na hatma yangu sijajua maana naendelea kusubiri tu na wala sijaelezwa kitu”.
Thania Msomali.
 Blog hii iliongea pia na Kiongozi wa wasanii katika kundi la Mashauzi Mr Hashim Said na kusema:-

"Fatma tulimuondoa ktk bend kwa utovu wa nidhamu, alitega kuja kazini kwa kisingizio cha kuumwa.

Yote hayo yametokana na siku hiyo ilikuwa ni alhamisi na bendi tuliigawa mara mbili baadhi walikwenda Mwanza kikazi na baadhi wakabaki Dsm kikazi waliokwenda mwanza waliambatana na Mkurugenzi waliobaki Dsm walibaki na mimi pale Mango Garden kikazi akiwemo Fatma! 

Lakini cha kushangaza Fatma alinitumia ujumbe muda wa saa moja usiku akidai anaumwa! Nikamuuliza huu ugonjwa umeanza saa hizi kwa kuwa ni muda wa kuja kazini? nikamwambia lazima aje kazini sababu waimbaji waliokuwapo ni wachache. 

Kinachoonekana ni kuwa Fatma alimaindi suala la yeye kubakishwa Dsm! La kushangaza zaidi kazini hakuja na akaonekana huko Mbagala akiwa na bendi hizi za mitaan akiimba hapo ndipo nilipomsimamisha kazi, kibaya zaid alishindwa kuomba msamaha Uongozi ukaamua kumuondoa katika bendi sababu hatuwezi kuwa na msanii asiekuwa na uzalendo na bendi yke! 

Thania nae tumemsimamisha kutokana na kiwango chake kila kukicha kinashuka na tumempa nafasi ya kufanya mazoezi zaidi ili akiwa vizuri basi atarudi kazini ".

Hiyo ndo habari kamili, kilichotokea hapo kimeongelewa ni Utoro/Utegaji na nidhamu ya kazi, wasanii kutokuwa na uzalendo na Bend zao.

0 comments:

Post a Comment