TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Saturday, March 1, 2014

BREAKING NEWS: Salha wa Hammer Q apata mtoto...!

Salha na Mwanae hapo pembeni!!
Msanii, mwimbaji mahili katika miondoko ya Taarab Tanzania Salha wa Hammer Q leo ameleta furaha ya ndoa katika nyumba kwa kujifungua mtoto wa kike.

Baba wa mtoto Hammer Q ambaye ni msanii wa kundi la mduara la Offside Trick aliiambia taarabuzetu.blogspot.com kuwa, mkewe amejifungua mtoto huyo wa kike leo tarehe 1/3/2014 mida ya saa nane (8:22) Mchana katika Hospitali ya Zakhem Mbagala.
"Mtoto kazaliwa akiwa na afya njema kabisa na tunamuomba Mungu amlinde na amkuze vyema mwanangu". Alisema Hammer Q

Blog hii inampa pongezi sana Mr & Mrs Hammer Q kwa kupata mtoto, Mungu awajalie kuwa na maisha mazuri mje kupata watoto wengine tena.

4 comments:

Anonymous said...

Pongezi nyingi sana kwa Salha na mumewe Hammer Q kwa kupata mtoto, maisha ni safari ndefu lazima kuvumilia milima na mabonde. Mwenyezi Mungu awajaalie mvumiliane ktk ndoa yenu ili mlee mtoto.

Anonymous said...

Hongereni sana na m.mungu awakuzie na mumlee mtt wenu ktk maadili ya kumpendeza allah (s.w).

Anonymous said...

Hongereni sana mung amkuzee amuondoleee maradhi amiiniii..

Unknown said...

nyimbo mpya za dar modern pliz mtuwekee tudownload

Post a Comment