TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Monday, December 16, 2013

Hammer Q apata ajali...

Hammer Q.
Msani wa kutumainiwa katika band ya 5Stars Modern Taarabu Hammer Q, jana (Jumapili) alipata ajali mbaya ya pikipiki.

Hammer Q aliandika katika ukurasa wake wa facebook kutokana na ajali hiyo:-
Leo (Jumapili) kwenye saa kumi jioni nimepata ajali mbaya ya pikipiki maeneo ya kwenye geti la Vikindu pale pale kwa anae pajua, nashukuru sikuumia hata kidogo.

Japo nimetoka kwenye tairi, namaanisha kilichonipa msaada wa kunyanyuka wakati nimedondoka Ni tairi ya pik up kwamba nikaishika na kunyanyuka ila ilikua inakuja maeneo ya tumboni na mwenzangu aliekuwa dereva ameumia sana.

Asante asante Mungu ni mara nyingi sana unanitoa hizo sehemu asante asante.

Taarabu zetu inampa pole sana Hammer Q, Mungu yu pamoja nawe...

0 comments:

Post a Comment