TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, December 11, 2013

KHADIJA KOPA KUFANYA SHOW YA NGUVU MOMBASA...

Khadija Kopa
Malkia wa mipasho nchini Tanzania Khdija Omary Kopa anatarajia kufanya onesho la nguvu mjini Mombasa siku ya tarehe 11 jumatano. 

Kopa ambae kaondoka jumanne hapa Dar kuelekea Mombasa tayari kwa onesho hilo amesema atafanya mambo makubwa katika show hiyo na watu watakubali kwamba yeye ni malkia!. 

Kopa aliyasema hayo nyumbani kwake mwananyamala anapoishi sasa baada ya kutoka katika nyumba ya marehemu mumewe Bagamoyo walipokuwa wakiishi enzi za uhai wake!. 

Amechukua nafasi hiyo kuwaomba wapenzi wake waje kwa wingi kupata burudani na kusikia wimbo wake mpya kabisa ambao watausikia kwa mala ya kwanza na hiyo kwa kwaajili ya watu wa Mombasa tu.

0 comments:

Post a Comment