TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Monday, December 16, 2013

Tamasha la Mitikisiko ndani ya Dar Live katika Matukio na Picha...

Ukumbi wa Burudani wa Dar Live usiku wa kuamkia jumapili ulitikisika kutokana na kufurika mashabiki ambao walijitokeza kwa wingi kushuhudia onyesho la Mitikisiko ya Pwani lililoandaliwa na Redio TIMES FM kwa udhamini wa Vodacom.

Bendi tano za miondoko ya taarabu zilitoa burudani ya nguvu ambayo iliwafanya mashabiki wa miondoko hiyo washindwe kutulia katika viti vyao. Zifuatazo ni picha kadhaa katika matukio tofauti, Kundi la Supershine ndo lilikuwa la kwanza kutoa burudani na Stail ya Ngoma ya Kimwera.

Mwimbaji wa bendi ya Super Shine, Queen Salma akifungua pazia la burudani.
Nuru Moshi wa Super Shine akitoa burudani.…
Waimbaji wa Super Shine wakiimba.
Ally J wa kundi la Five Star akiimba jukwaani.
Maua Tego wa Five Star akitoa burudani...
Khadija Kopa (Kati) akicheza na waimbaji wake.
Fatma Machupa wa Jahazi akifanya vitu vyake.
Fatma Mahamud wa Jahazi akitoa burudani kwa mashabiki...
Mkurugenzi wa Mashauzi Isha Mashauzi na mdogo wake Saida wakifanya kazi iliyowapeleka ukumbini, yaani burudani tu.
Waimbaji wa Mashauzi Classic wakiimba...
Hashim Saidi Igwee akifanya vitu vyake jukwaani...

MC wa Shughuli nzima, Dida akiwakilisha kazi yake...
Mashabiki alijitokeza kwa wingi kupata burudani ya uhakika... Full Bata...!!


1 comments:

Unknown said...

kwakeli makundi machache ndio yamefanya vizuri lakini la mwisho halukutenda haki kwa washabiki

Post a Comment