TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, December 11, 2013

MATUSI YAMEZIDI KWENYE TAARABU...

Bendi ntingi za taarabu nchini zimedaiwa kuimba matusi katika nyimbo zao.
Blog ya taarabuzetu.blogspot.com imepokea malalamiko kadhaa toka kwa mashabiki wa mziki huu wengine wakitoa dukuduku zao katika page mbalimbali za facebook.

Wengi wamelalamikia nyimbo kuwa na mashairi makali sana na matusi yasiyofichika kwa mtu anayejua vyema kiswahili, na wengine kudai kuwa wengi wa wasanii wa taarabu wamekuwa wakiimbana wenyewe tu badala ya kuleta burudani ya mashairi mazuri na matamu kama zilivyo nyimbo za waimbaji wa zamani.

Hapa ni baadhi ya msg za wadau:-



AbbaMouk J kiukweli bila upendeleo wala chuki! Funga kazi nyimbo zao hazina mahudhui ya mziki wa taarab! kunanyimbo waliamba cjui nan machupa ndg yake rahma machupa! watu wengi waliokua wakiuona kwny tv waliuponda na kusema kama taarab zmeanza kua hv bas hata kwenyenyumba yng hazitoingia nakumbuka mara ya kwanza nmeuona nlikua npo singida sasa tulikuwa kwa mwenyeji wetu ndy ulirushwa ktk kipindi cha #Hawa_Hassan cha I T V,ukija kwa huo nzi wa kijani leo hii nlikua nachat na mtu alikua akiniuliza khs mambo hayo hayo ya mziki wa taarab akaniuliza hv umeusikia wimbo wa nzi wa kijani? nkamwambia bado kwahiyo hata huujui hata mashair yake? nkamwambia sijabahatika kuusikia akanambia sijapenda mashair wala uimbaj wao sikuweza kumuunga mkono cz sijawah kuusikia so wasanii wanatakiwa wanapoumiza vchwa vyao kutunga mashairi wajaribu kuweka chuki zao pembeni na kutumia mda wa ziada kujaribu kuchambua ni matukio yep yanaendana na jamii hata km unamjibu mpinzani wako lkn maudhui yasitoke nje ya kile ulichokikusudia.

Tende Mikidadi Sheshi Huo Wimbo Wa Inzi Wa Kijani Cjausikia Bado Lkn Kila Aliewahi Kuusikia Anasema Haufai,,Sasa Jiulize Kwanini Kila Mtu Anasema Haufai ?Unajua Vijembe Vipo Kwenye Taarab Lkn Visiwe Live Au Uijibu Nyimbo Ya Mtu Kiasi Hata Mtoto Akiusikia Anajua Umemjibu Fulani,,Binafsi Sipendi Nyimbo Za Aina Hiyo,,Halaf Zamani Ilikua Ushabiki Wa Band Lakini Siku Hizi Msanii Akishea Bwana Na Msani Mwenzie Kesho Kamtolea Nyimbo,,Ndomana Kuna Msemo Mtaani Kuwa Taarab Ni Mziki Wa Uswahilini,,Umejaa Umbea Na Vijembe Japo Si Kweli Hivyo Watunzi Mjiangalie ,Hatutaki Kuimbiwa Mambo Yenu Binafsi ,Tunataka Maudhui Yanayogusa Kila Mtu .

Amin Salmin Sheshi beshi ushairi wa tembe tumepishana sana wake ndio una matusi ya nguoni,ushairi wangu kwa nyimbo za mipasho huwa na pasha na kazi ya mipasho ni kupasha upashike ila hakuna matusi kwa mfano,Naona umepagawa,wenda mbio kila uchao,kiwewe kitakuuwa,sina wasi wasi mwenzio,hilo lako la rohoni daima lita kukerekata,kosa sio langu mm,mumeo ndotoni kunitaja,huna bizi we mzushi,is wa hamsini wala mia,hayo kwangu matapishi, ww unayojivuni,Ukiangalia kwa undani huo ni mpasho na sio nyimo ya tauhidi.

Sheshi Beshi Amin swadakta temba anatumia matusi na wewe mipasho yako iko live ndio nikasema mbinu ya tafsida kwenu ipo chini, huyu hajui ku2mia maneno mbadala ya visawe na wewe ku2mia mafumbo pia hujui, ila mm cna tatizo nasema tena hiyo ni feedback tu.

Tende Mikidadi Tatizo Baadhi Ya Watunzi Wanatunga Nyimbo Wakiwa Na Hasira Basi Hapo Hapo Anashika Kalam Na Kuaza Kuchamba Maana Si Kutunga Tena ,,Iko Cku Mtu Ataimba We Ms**ng Koma Na Mie,,Nadhani Hapo Serikali Itatangaza Kupiga Marufuku Muziki Wa Taarab Na Tabid Sasa Watu Wahamie Dansini Au Kuigiza Movie,,Ila Jamani Mi Nalia Na Mashairi Makali Yanini ?Halaf Kila Mtu Anajua Kabisa Kaimbwa Mtu Fulani,,Mbona Majanga ? 

Hizi ni baadhi ya Comment za watu wakiongelea mashairi ya Taarabu...

Wewe kama mdau unalizungumziaje hili suala la matusi na Vijembe vya waziwazi na kuwekeana mabifu!? 

1 comments:

Anonymous said...

hao sio watunzi ila wamevamia fani yaani mpaka taarabu naichukia sasa,waige mfano wa mzee anajibu kimafumbo bila matusi mfano wimbo wa sitaki shari una maudhui madhuri,lkn amin salmin hajui mafumbo .

Post a Comment