TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Monday, December 16, 2013

Je!, Nisahihi kwa msanii wa Taarabu kwenda kuimba katika Band nyingine isiyo ya kwake.

Hili hapa ni swali kutoka taarabuzetu.blogspot.com kwenda kwa wamiliki na wadau mbalimbali wa Taarabu hapa Tanzania, baadhi ya watu waliohojiwa na mwandishi walijibu kadri wajuavyo.

Swali na majibu yake ni hayo hapo chini:-

SWALI:-
Wasanii wengi wa Taarabu wamekuwa wakiwayumbisha sana mashabiki wao wasijue leo msanii huyu atakuwa wapi kutokana na tabia ya kwenda kuimba katika Show yoyote ya bendi za Taarabu na wakati yeye anatumikia bendi nyingine.

Hivi hii ni sawa au huwa ni makubaliano katika mkataba?
Kwanini wasanii wasitulie na kuhudhulia katika show za bendi yake tu!?

Naomba unifafanulie na unipe maoni yako ili nami niweze kuwajulisha wasomaji na wapenzi wa Blog ya Taarabu Zetu, Tafadhali...


Amin Salmin
Amin Salmin (Boss T Moto Modern Taarabu):-
Ok hapo kuna namna mbili:-
1. Na ndio kubwa zaidi ni kutokana na bendi anayoitumikia kutokua na maonesho kwa namana moja au nyingine na km unavyojua maisha magumu.

2. Hii ni zaidi kwa wale wasanii mastar au wenye uwezo wakati bendi ambazo hazina mastar hupenda kuwatumia kama mgeni mualikwa lkn kubwa ni kukosa kwa show ktk bende wanazo zitumikia na hali ya maisha.

Taarabu Zetu:-
Hivyo kwa upande wa wamiliki wanawaruhusu tu kwa vile hawawalipi vizuri kutokana na maelewano yao au?

Amin Salmin:-
Hapana unajua bendi zote hua hawalipi mshahara ikimaliza show kila msanii analipwa kutokana na viwango,so km itatokea atapata day work anakwenda nako analipwa vile vile akimaliza tu na hii ni kuhofia mivutano mwisho wa mwenzi.


Amani Mbilo
Amani Mbilo (Mtangazaji Bomba FM - Mbeya):-
Kwa mtazamo wangu kinachochangia:-
1. Ni kutoka na na wasanii wengi kuwepo kwenye kundi pasipo na mikataba ya uhakika usiyowabana

2. Masalahi ndio chanzo kikubwa wasaani wanaona ni bora wahaangaike wenyewe kwa kuwa mishahara midogo

3. Tamaa tu na kutokuwa na subira ya kuweza kukakaa katika band yake na kusubiri mshahara na posho wanazopata

4. Wasani wengi wanaamini show ndio zitakazo watambulisha na nyimbo zao kupendwa kupitia hizo shoow hivyo basi wanalazimika kufanya show nje ya band zao, Hawatutendei haki mashabikiiii.

Taarabu Zetu:-
Vizuri sana Amani, hivyo unashauri vp!? Wakae katika bendi bila kwenda kupiga show katika bendi zingine au waende tu kutokana na mishahara kuwa midogo kama ulivyosema?.

Amani Mbilo:-
Watengenezewe mikataba mizuri na ya haki, na walipwe vizuri ili watulie katika band zao.



Mgeni Kisoda
Mgeni Kisoda (Mpiga Kinanda 5Stars):-
Kaka maisha tu.

Taarabu Zetu:-
Kaka maisha yanafanya nini?

Mgeni Kisoda:-
Ndiyo yanayo mfanya mtu ahangaike...




Hamis Slim
Hamis Slim (Boss G5 Modern Taarabu):-
Huwa ni makubaliano kati ya mwenye bendi na msanii wake kwani wasanii wengine kwa siku asiposhika maiki huwa anahisi kama anaumwa.

Mwingne ni katika kuhitaji muonekano sizani kama kuna msanii ambaye ametoka kisanii utamkuta katika stage ovyoovyo zaidi akialikwa tu, sasa kwa hawa wengine huwa wanashindwa kutumia fursa wanazopewa na mabosi zao kuwa anaweza kuimbia bendi yoyote endapo amealikwa ili azidishe kukuwa kwake kisanii lakini sio kwenda kuimba na kukaa ktk stage ya bendi fulani wakati uko kwenye bendi nyingne ile unajizalilisha kama msanii na hata ile bendi yenyewe pia inaonekana haina uwezo wa kuibua vipaji vya wasanii wanategemea wasanii wa bendi zingine ni hivyo kaka hakuna zaidi ya hayo itakuwa uongo tu.

Taarabu Zetu:-
Kaka wengine wanadai masilahi ni kidogo mno ndo maana wanatoka nje kujitafutia, na kwavile maboss wanawalipa kidogo wanashindwa kuwazuia!! Vipi kuhusu hilo? Na kuhusu mashabiki wafanyeje katika ushabiki!?

Hamis Slim:-
Kwa maslahi kaka hilo cna uthibitisho nalo coz hakuna binadamu anayetosheka na pesa kaka mfano wasanii wa Jahazi ushawaona ktk majukwaa ya bendi nyingine? na wafanya vile ni kwa utaratibu wa boss wao lakini ckama wana maslahi makubwa la hasha.

Pili mbona wengine huwa hawafanyi hivyo na wapo ktk bendi wanazotoka hao wanaofanya hivyo au maslahi ni kwa hao wanaofanya hivyo tu ndio wanaojua maslahi?

Ndo maana nikakuambia kuhusu mengine uongo coz nilijua utakuja ktk swali hili 7bu wasanii nawajua anaweza kupewa pesa ya mkataba laki 5 na akatangaza kapewa milioni 5 baada ya muda anaanza visa mwishowe anakuambia maslahi!, je hili nalo unalichukuliaje!?

Taarabu Zetu:-
Dah!. Hiyo nayo ni kweli kabisa mkuu!! Jahazi wanautaratibu wao, maana hata kama una mapenzi ya kumuona msanii fulani ni lazima uende Jahazi na si kumsubiri katika bendi nyingine ili umuone. Msimamo unahitajika ili heshima ipatikane.

Hamis Slim:-
Yah! maboss wengine huwa hawataki kuwabana wafanyakazi wao co wanamuziki tu tatizo cc watanzania huwa hatujitambui nahatujui nn maana ya uhuru au nn haki za mfanyakazi kwa boss na nn haki za boss kwa mfanyakazi mara nyingi huwa zinaangaliwa haki za mfanyakazi kwa boss tu.


Hashim Said
Hashim Said IGwee (Kiongozi wa Wasanii Mashauzi):-
Kimtazamo wangu si mbaya kufanya hivyo ila haipendezi kwenda kuimba bendi nyingine cku ambayo bendi unayofanyia kaz iko ktk parfomance inatakiwa cku zile ambazo huna show si mbaya kwenda kusalimia jukwaa la bendi nyingine.

Mfano mimi hapa huwa kila jumatatu nakwenda lango la jiji magomen ambako hutumbuiza bendi ya EAST AFRICAN MELODY nakwenda kwa sababu cku hyo niko free lakini cku zingine huwez kunikuta bendi nyingine labda tusiwe na onyesho pahala.

Taarabu Zetu:-
Kwa upande wa mashabiki wako kaka wakufuate wewe au Mashauzi na East African Melody!? Na unaonaje mkitulia tu Bendi moja!?

Hashim Said IGwee:-
Mashabiki wangu nashukuru nnapokwenda Melody kutembea huwa wanakuwepo na hufurahia nnaposhirikiana na wasanii wenzangu ikumbukwe kwamba nilianzia Melody ndio nikaja Mashauzi wengi wa mashabiki wanalifahamu hilo huwa nakwenda pale kutembea siku ambazo niko off kikaz.


Warda Chande.
Warda Chande. (Mtangazaji - Passion FM):-
Kwakweli, it depends na mkataba ulivyo kama unamruhusu msanii kufanya kazi za nje kwa mda wa ziada baada ya kazi za Band (Siku ambazo band haipigi wala mazoezi hakuna) sio mbaya ni kutokana na hali halisi ya kimaisha mtu (Msanii) anaamua kufanya hivyo ili kuweza kuendesha maisha yake.

Lakini kwa upande mwingine kama mkataba wake haumruhusu kufanya hivyo na mwenyewe ameweza kusaini kwa mkono wake inabidi asifanye kazi nje ya band yake kwani atakuwa amekiuka mkataba (atakuwa kinyume na Mkataba).

Ushauri wangu kwa wamiliki wa band ni kuwapa uhuru wasanii wao kufanya kazi nje ya band kwa muda ambao band haifanyi kazi (Show) kwasababu hali halisi ya maisha inajulikana ni ngumu .
Kwa upande wa mashabiki inabidi tuelewe wasanii wapo katika kutafuta so kikubwa zaidi ni kupata burudani nzuri kutoka kwa msanii haijalishi katoka band gani au ni solo artist au leo yupo hapa na kesho unamuona pale, kikubwa ni kupata burudani (Kuburudika na Kuelimika.



Kais Mussa Kais
Kais Mussa Kais (Meneja - Supershine):-
Unajua kaka kuna ule urafiki kati ya bendi kwa bendi na msanii kwa msanii. Kwahiyo sio mbaya kwa msanii kwenda ktk bendi ingine na kuimba ni just urafiki kisanaa, lakini issue inakuja pale msanii anapoonekana ktk show zaidi ya tano au kumi za bendi nyingine tofauti na kule alipoajiliwa hili ni tatizo na limekuwa likifanywa sana na wasanii wa taarabu wenyewe wanaita "NDONDO" sio nzuri inawayumbisha wapenzi wasijue huyu msanii ni wa bendi gani haswa?.

Imefika wakati kwa viongozi wa taarabu kukemea jambo hili kwa ajili ya kuleta heshima kati ya bendi na msanii husika ni hayo tu!.




Kisolo Mwanamarui
Kisolo Mwanamarui (Mpiga Solo - Mashauzi):-
Kaka kuhusu swali lako ni zuli sana nikweli wasanii sasahivi wanaacha band zao nakwenda kufanya show kwingne tena hadi wamiliki waband wenyewe wenye majina hufanya hevyo kwaheyo kwakweri tunawayumbisha mashabiki ilakwa sisi wapigaji Vinanda ndio hatufanyi hivyo.

Mi nasema wasani tupunguze tamaa ya pesa tuendeleze muziki na bendi zetu kwani tuko juu kwasasa.




> > > > >    < < < < <

Hayo ndo maoni tuliyopata.
Mziki wa Taarabu sasa unazidi kukua na kukomaa, sisi kama wadau wakubwa wa mziki huu wa mwambao tunaomba wamiliki na wasanii wote kufikiri kwa makini jambo hili ili lisije kuwayumbisha, ni kama vile haijakaa vizuri kutokana na maoni hapo juu.

0 comments:

Post a Comment