TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Friday, January 24, 2014

5Stars ipo mikononi mwangu kwa sasa - Ally J

Mtangazaji wa Passion FM Warda Chande akiwa na mcharaza kinanda wa 5Stars Ally J.
Baada ya aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa 5Stars Mr. Shark's kuivunja Bendi yake na vyombo kuvifungia ndani na kisha kuwapa wasanii wote uhuru wa kwenda wanakotaka, Ally J ameamua kuichukua bendi ili aiendeleze.

Ally J ameyazungumza hayo akiwa anahojiwa na Blog hii pamoja na mahojiano ya moja kwa moja na mtangazaji wa kipindi cha Taarabu "Ambaa na Mwambao" Passion FM Warda Chande.

Amesema kuanzia sasa Bendi ipo mikononi mwake baada ya kukaa na aliyekuwa Mkurugenzi Mr. Shaks na kuyamaliza.
Ally J akionesha manjonjo yake katika kusakata muziki wa Mwambao.
Kinachofuata kwa sasa ni kuvumiliana tu, Bendi ipo itakuwa imara kama mwanzo, kama kawaida na wasanii wote wapo imara kuendeleza Bendi hivyo hakuna kitakachoharibika wala kupungua.

Ally J ambaye ni mpiga kinanda mkongwe aliyewahi kupigia bendi mbalimbali hapa nchini amechukua uamuzi wa kuiendeleza bendi kwa mapenzi yake makubwa huku akiomba wito kwa wadau wa Taarabu na wenye nia ya dhati kuiendeleza 5Stars kuwa wajitokeze ktk mazungumzo ya Udhamini kama ilivyokuwa kwa Shak's.

Wapenzi wote wa 5Stars wasiteteleke bali wasubiri tu ujio mpya kwa sura na sauti zilezile.

0 comments:

Post a Comment