TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, January 22, 2014

TETESI:- BAADA YA 5STARS KUVUNJWA BENDI MBILI ZINGINE KUFUATA

Mkurugenzi wa T Moto Amin Salmin akiwa na Jokha Kassim.
Baada ya Bendi maalufu na iliyokuwa juu kimziki 5Stars Modern Taarabu kuvunjwa kuna bendi zingine mbili (2) zipo mahututi au zimekufa kimyakimya.

Baadhi ya wapenzi wa Taarabu hapa nchini na sehemu mbalimbali Duniani wanaopitia katika blog hii ya taarabuzetu.blogspot.com wamekuwa wakituma msg, Email na simu kuulizia hatma ya baadhi ya makundi ambayo hawayasikii kwa sasa.
Mwandishi wa blog hii pia amekuwa na mashaka kidogo kitu ambacho kilimfanya aanze kufanya uchunguzi wa suala hilo.

Tumeongea na baadhi ya wasanii wa bendi ya T Moto Modern Taarabu na kusema kuwa hawana Show bendi yao kwa muda mrefu sasa na wamekuwa wakihaha sehemu ya kujipatia riziki na kuhudumia familia zao. "Bendi ipo haijafa kwasababu hatujatangaziwa hivyo ila ndo hivyo hatuna show hata moja kitu kinachotufanya tuishi maisha ya kukosa ajira. Mmoja wa wasanii alifunguka.
Mwandishi wa blog hii anafanya mawasiliano na Mkurugenzi wa T Moto ili aweze kufunguka naye kuhusu hatma ya wasanii wake.

Wasanii wa Bendi ya Fungakazi Modern Taarabu.
Bendi nyingine inayoonekana kuzama ni Fungakazi Modern Taarabu iliyo chini ya Mkurugenzi Kaptain Temba.
Inadaiwa bendi hii haina wasanii kwa sasa kwasababu hawakutani kwa show wala kwa maongezi yoyote, inaonesha bendi imekufa au inaelekea pabaya.

Wasanii wa Fungakazi Modern Taarabu kwa sasa hawasikiki na hawafanyi show yoyote hapa mjini, kwahiyo inaonesha hawana ajira.

Wakurugenzi wa T Moto na Fungakazi mnaombwa na wapenzi wa Taarabu pamoja na wasanii wenu kufanya mpango wa kuendeleza Bendi na kupanga Show kama ilivyokuwa mwanzo.

0 comments:

Post a Comment