TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Monday, January 20, 2014

BENDI YA 5STARS IMEVUNJWA, ANAYETAKA VYOMBO AKANUNUE, ANAYEMTAKA MSANII AMCHUKUE...!!

Baadhi ya wasanii waliokuwa wakiunda kundi la 5Stars
 Kundi maarufu la mziki wa mwambao Tanzani 5Stars limevunjwa na wasani wapo huru kwenda popote.

Akizungumza na Blog hii aliyekuwa mmiliki wa Bendi hiyo Mr. Shaks amesema Bendi amevunjwa hataki tena kusikia mambo ya Bendi, amechoka na anataka kufanya mambo mengine sasa.

Mr. Shanks aliendelea kwa kusema sababu zilizomfanya aivunje Bendi ni kutoona faidi yake toka aanzishe na imekuwa kero kwake kwa kerere za wasanii kila siku, ameamua kuvunja mikataba ya wasanii wote pamoja na kwamba wengine alikuwa nao kwa mikataba ya muda mrefu kama miaka miwili (2) "Bora nipate hasara hii kuliko kuendelea kupata hasara" Alisema.

Aysher (Vuvuzela) na Mgeni Kisoda.

"Kwasasa sitaki mtu aniambie kitu chochote kuhusu Bendi, wasanii nimewapa uhuru mapema waweze kwenda kokote wanakotaka na mimi nifanye mambo yangu mengine
Mwenye Kuhitaji vyombo vya mziki anitafute tufanye biashara na kama atahitaji jina la 5Stars nitampa ila mimi basi". Shaks alisema.

Hammer Q Na Salha
Kwa habari zadi kuhusiana na kuvunjwa kwa 5Star tutasikia wasanii wanasemaje.
Tuvumilie kidogo.




4 comments:

Unknown said...

jamani ushirikina upooooooooo, misukosuko yote alokumbana nayo leo ndo anaamua haya..na vile walikua wanakuja kali..

Anonymous said...

Daaah yan cna l kusema mie imeniuma snaaa

Anonymous said...

Daaah yan cna l kusema mie imeniuma snaaa

Anonymous said...

JAMANI 5STARS TULIWAPENDA SANA SIJUI ITAKUWAJE TENA...

Post a Comment