TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Monday, February 17, 2014

TWAHA MALOVEE ATANGAZA KUIACHA RASMI DAR MODERN....

Muimbaji machachali na wa kutumainiwa ndani ya Dar Moder Twaha Malovee.
Muimbaji tegemezi na wa siku nyingi ndani ya bendi ya Dar Modern Taarab Twaha Malovee, amejitangaza rasmi kwamba yeye kwa sasa si msanii tena wa bendi hiyo na ameamua mwenyewe kuacha wala hajafukuzwa na kiongozi yeyote yule.

"Ndugu mwandishi nimeacha kazi Dar Modern na sina kinyongo na mkurugenzi wangu, FERESH namshukuru sana amenisaidia sana tena sana nampongeza kwa huruma yake kwa wasanii!. Unajua pale kuna ubaguzi unafanywa na kiongozi mmoja alieletwa kubagua wasanii aliowakuta na kuwapa kipaumbele zaidi wale aliowaleta yeye.
Mimi ni bonge la muimbaji najitambua siwezi kuburuzwa nimeamua kuacha bendi ili waendelee na nawatakia maendeleo wafike mbali. Kwa sasa nipo katika mazungumzo na bendi moja kubwa ya taarabu na wakati ukifika kila kitu kitakaa sawa na wapenzi na wadau wangu nitawafahamisha" alimaliza kwa kusema.

Wiki iliyopita Twaha aliibukia katika jukwaa la Supershine na kuimba nyimbo moja, baada ya hapo alipomaliza kuimba alijitangaza rasmi kuacha kazi Dar modern nakuwaambia wapenzi na mashabiki zake kwamba wasijisumbue kumfuata katika uzinduzi wa albam mbili za bendi hiyo uliofanyika Travetine Magomeni kwani hatokuwepo jambo lililotafsiriwa na wapenzi kwamba labda Twaha ana mpango au yupo njiani kujiunga na kundi hilo la Supershine Modern Taarab.

Tusubiri tuone Twaha atajiunga na bendi gani!!.

0 comments:

Post a Comment