TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Saturday, February 15, 2014

UZINDUZI WA ALBAM MBILI DAR MODERN WAFANA...

Waimbaji wa Dar Modern Taarab wakiwajibika jukwaani.
 Bendi ya Dar Modern Taarab yenye makazi yake jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo walifanya uzinduzi wa albam zao mbili kwa mpigo katika ukumbi wa Travertine Magomeni.
Albam zilizozinduliwa ni: "KITWITWI" NA "NGOMA IMEPASUKA".

Ilikuwa ni kama picha ya Kihindi watu wakitegemea siku ya mwisho sterling anakufa lakini sivyo ilivyokuwa.

Pamoja na kuwepo na burudani katika ukumbi wa jirani wa LANGO LA JIJI toka kwao East African Melody lakini Wana wa pembe la Ng'ombe walijaza watu isivyo kawaida.

Shukrani ziende kwa uongozi mzima wa Dar Modern kwa kufanya maandalizi mazuri.
Mnenguaji wa Baikoko akifanya yake.
Show ilianza saa 3 kama ilivyo ada na walioanza kuleta raha ni BAIKOKO ambao walichengua mashabiki vilivyo na kuwafanya washindwe kukaa vitini!

Baada ya hapo waliingia wenyewe wenye shughuli nikimaanisha Dar Modern ambao walipiga nyimbo tatu mfululizo zilizowafanya watu kumwagika jasho kwa kucheza.
Wasanii wa kundi la Kibao Kata wakiburudisha mashabiki.
Ilipofika saa sita usiku walipanda wana Kibao Kata ngoma yenye asili ya mkoani Tanga nao walipiga nyimbo zao 3 mfululizo na kuwafanya mashabiki wao kupiga mayowe wakiomba kuongezwa kwa wimbo mwingine toka kwao.
Waimbaji wa Dar Modern - Mwanvita Shaibu, Zubeda Mlamali na Mosi Suleiman.
Katika raundi ya mwisho walipanda tena Dar Modern Taarab wakiongozwa na Bi Mwanahawa ally ambae aliwapa wapenzi wake burudani ya nguvu, baadae walipanda wasanii wengine kama Zubeda Mlamali, Mosi Suleiman, Hasna Mlamali, Mwamvita Shaibu na wengineo.
Waandishi wakikabidhiwa CD za Nyimba.
Ukumbi ulikuwa umefurika mbayaa...!!
Mashabiki hawakukaa kadri burudani ilivyokuwa ikiendelea ukumbini hapo...!
Show ilimalizika saa kumi kasoro za alfajiri na kuwafanya wapenzi na mashabiki wa Dar Modern kulidhika na kushusha pongezi za nguvu kwa wasanii na viongozi kwa ujumla.

Bendi hiyo itakuwa ikitumbuiza katika ukumbi huo wa Travetine Magomeni kila ijumaa ilikuwapa burudani wakazi wa Magomeni na vitongoji vyake mfano kama Sinza, Mwananyamala, Manzese na sehemu zingine za karibu.

Tunawaahidi kuwawekea nyimbo zao mpya ili muweze kuzisikiliza na kuzi-download!.
Hongereni sana Dar Modern kwa kazi nzuri mliyoifanya.
BIG UP SANA!.

0 comments:

Post a Comment