TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, October 29, 2013

AISHA VUVUZELA AIACHA SOLEMBA KING'S MODERN TAARABU...


Msanii muimbaji anayekuja kwa kasi katika tasnia ya muziki wa taarabu Aisha Othman "Vuvuzela" ameiacha solemba bendi ya King's na kutimkia 5Stars Modern Taarabu.

Taarabuzetu, tuliandika kwa mara ya kwanza juu ya taarifa juu ya Aisha Vuvuzela kwenda katika kambi ya 5 Stars kusaini mkataba na hadi muda ambao alikwenda tuliandika kwa ushahidi kabisa, lakini baadhi ya blog na media zilikanusha na kusema habari hizo sio za kweli. 

Leo hii mtandao wako makini wa taarabuzetu.blogspot.com unakuletea hitimisho la sakata zima lilivyo malizika. 

Mpaka sasa VUVUZELA ni msanii halali kabisa wa bendi ya 5 Stars na amesaini kuitumikia bendi hiyo kwa miaka miwili.

Taarabuzetu ilimtafuta mkurugenzi wa 5 Stars Mr Sharks ili kuthibitisha hili.
 Akiongea na mwandishi wetu, Mkurugenzi huyo alisema:- 
"Napenda kuchukua nafasi hii kuwathibitishia wananchi wote kwamba Aisha Othman "Vuvuzela" ni msanii wangu halali na nimemsainisha kwa muda wa miaka miwili, alipokuja aliniambia kwamba hana mkataba na bendi yake ya awali ya Kings ndipo nilipo msainisha kuitumikia bendi yangu, na muda huu tunavyo zungumza VUVUZELA yupo katika bendi yangu na ni msanii wangu kihalali". 

Alipopigiwa simu mkurugenzi wa bendi ya Kings Modern Taarabu kuulizwa juu ya kuondoka kwa msanii wake huyo, alijibu.. "Nina mkataba na VUVUZELA na nitachukua hatua kali dhidi yake ili kukomesha hili".

0 comments:

Post a Comment