TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, October 9, 2013

TETESI:- 5 STARS MODERN TAARABU KUITWA "V.I.P. MODERN TAARABU"...!!

Baadhi ya wasanii wa 5Stars Modern Taarabu wakiwa kazini.
Siku zote unapoona mtoto anakuwa mtundu, hasikii la kuambiwa, mkorofi n.k, wazee wa zamani watakwambia mtoto jina linamzuru mbadilishe jina atatulia! na kweli unapombadilisha mtoto anakaa sawa na kila kitu kwa upande wake kinakwenda vizuri. 

Bendi ya 5 Star's ni miongoni mwa bendi zilizokuwa zikifanya vizuri katika soko la taarabu mpaka kufikia kuogopwa na zile bendi zinazojiita kongwe hapa nchini. 

Bendi hii ambayo hapo mwanzoni ilikuwa na wasanii mahiri kama Ally J, Issa Kijoti, Shebe Juma, Tizo Mgunda, Husna Mapande na wengineo, ilipata ajari mbaya sana iliyopelekea wasanii 13 kufariki. 

Baada ya hapo bendi ilianzishwa upya chini ya mkurugenzi mpya Mwandame mkazi wa Mwanza na walifanikiwa kutoa albam mbili chini ya Director Ally J lakini bado bendi ilionekana kutokubalika kwa washabiki tena kama ilivyokuwa mwanzoni, jambo hili lilimfanya mkurugenzi Mwandame kuitosa bendi hii kwani aliona anapata hasara tu ukizingatia yeye aliwekeza ili apate faida na sivinginevyo. 

Baada ya hapo bendi ilinunuliwa na mkurugenzi Shark's ambae nae hakuona manufaa yoyote ndipo bodi ilipokaa na kuamua kubadilishwa kwa jina na kuitwa "VIP MODERN TAARABU", jina hili la Vip Modern Taarabu, Inasemekana limechomoza mapema mno tofauti na ilivyopangwa kwani inaonekana baadhi ya viongozi hawana siri, mtandao wetu ulimtuma kachero wetu katika kambi hiyo na kukutana na mmoja wa viongozi wa bendi hiyo ambae alisema kwamba kweli hilo jina lilipendekezwa lakini bado halijapitishwa rasmi tusubiri tuone kwani itakapokuwa sawa kila kitu kitawekwa bayana lakini mpaka sasa bado bendi inaitwa 5 Stars Modern Taarabu. 

Wasomaji wa blog yetu tunawaahidi kuendelea kufuatilia jambo hili na tutawaletea hapa hapa tusubiri, pia kwa uongozi wa 5Stars kama watapendekeza jina hili ni zuri kwakweli na linaonekana kuwa na Mvuto kabla ya kuanza kutumika, Taarabu Zetu imelipenda...!!!

0 comments:

Post a Comment