TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Monday, October 7, 2013

KHADIJA KOPA KUMALIZA EDA TAREHE 14/10/2013.

Khadija Kopa. "Malkia wa Mipasho".
Khadija Omary Kopa au malkia wa mipasho nchini Tanzania, anatarajia kumaliza EDA yake mwezi huu tarehe 14 na rasmi anaanza kazi tarehe 19 akiwa na kundi lake la TOT ndani ya ukumbi wa DAR LIVE Mbagala jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa simu akiwa kwake Bagamoyo, malkia huyo alisema nitaendelea kumkumbuka na kumuenzi marehemu mume wangu kwani ni pigo kubwa ameniachia na pengo lake halizibiki kwakweli, Jafary upendo wake kwangu ulikuwa hauna mfano, mwenyezimungu amlaze pema peponi mume wangu!. 

Wapenzi na wadau wa Adija Kopa mjiandae kumpokea!

1 comments:

Unknown said...

jamani Taarabu zetu nawaombeni siku malkia wa mipasho Khadija kopa akifanya show Dar live mutuwekee clip humu ndani tuone katoka vp

Post a Comment