TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Thursday, September 5, 2013

ASILI YA TAARABU IMEPOTEA KABISA NCHINI..YAMEBAKI MADEBE TUPU!!... SITI BINTI SAAD AKUMBUKWA...

Siti na kikundi chake walipoenda Mumbai (Bombay), India kurekodi santuri kadhaa mwaka 1929.
Siti Binti Saad 1880-1950

Wakati Mohamedy Liasi anaimba kamwe huwezi kuchoka kumsikiliza, Siti Binti Saadi anapoimba kwa hisia chozi linaweza kukutoka na usijue limekutoka muda gani! hiyo ndio taarabu tuliyoizoea sisi alisikika mzee Kampira wa mwananyamala Dar es Salaam akilalama namna hiyo!. 


Mwandishi wa habari hizi alitaka kujua nini sababu haswa zilizopelekea yeye kuzungumza yote hayo?, akaendelea kusema ni juzi tu hapa niliamua kutoka na familia yangu kwenda hapo Travertine Magomeni kaitak Taarabu, basi nilichokutana nacho nilijilaumu kwanini nilikwenda yaani uchafu mtupuu!! si ile Taarabu niliyotegemea na niliyoizoea.

**********

Mwimbaji maarufu wa Tanzania, Malkia Original wa Mipasho, Siti Biti Saad afariki dunia mwaka 1950..

Siti alizaliwa katika kijiji cha Fumba huko Zanzibar. Jina aliyopewa na wazazi wake ilikuwa Mtumwa. Wazazi wake walikuwa watumwa kutoka Bara.

Aliishi maisha duni hadi alipohamia mjini Zanzibar na kuanza kupata umaarufu wa kuimba Taarab. Watu walimfurahia kwa vile alikuwa anaimba taarab kwa kiswahili lugha ambayo walikuwa wanatumia hasa ilikuwa kiaarabu.

Sultan alimwalika kuja kumwimbia. Baadaye alifanikiwa kwenda India na kikundi chake kurekodi santuri. Enzi zile zilikuwa zile 78's. Vijana wa siku hizi hawawezi kuzijua.

0 comments:

Post a Comment