TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, September 4, 2013

SUPERSHINE MODERN TAARABU KUINGIA STUDIO JUMATATU..

Ally Mikidadi.

Bendi ya supershine modern Taarabu inatarajia kuingia studio siku ya jumatatu kurekodi nyimbo zao 2 ili kukamilisha albam mpya itakayokuwa na nyimbo zipatazo 5. 


 Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, meneja wa bendi hiyo Kais Mussa Kais alizitaja nyimbo hizo zitakazorekodiwa jumatatu kuwa ni: 
1. "Usia wa baba" - Utaimbwa na Queen Salma na Ally Mikidadi
 2. "Wafadhiraka wa pundaka" - Utaimbwa na Bibie Nuru Moshi

Nuru Moshi.
Nyimbo hizo ambazo ni moto wa kuotea mbali zitakamilisha idadi ya nyimbo 5 mpya za supershine. na albam itabeba jina la "Huna style" wimbo alioimba Queen Salma!. 

Supershine ni bendi iliyokuja kivingine na kwa kasi zaidi chini ya Meneja wake Kais Mussa!.

0 comments:

Post a Comment