TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, September 29, 2013

*SHINDANO LA KIGOLI * MZEE YUSUPH AIKACHA G5 MODERN TAARABU...

Mzee Yusuph.
Lile shindano la kigoli ambalo linaandaliwa na mwanadada maarufu hapa jijini Dar MAIMATHA limezua kasheshe baada ya mfalme Mzee Yusuph kukataa kupanda jukwaa moja na bendi ya G5 Modern Taarabu.

Akizungumza na mtandao huu chanzo chetu cha habari kilieleza kwamba muandaaji aliamua kuwashirikisha G5, Karunde Bend na msichana DYNA ili kunogesha zaidi shindano lake lakini alikutana na kipingamizi kikubwa toka kwa Mzee, inasemekana Mkurugenzi huyo wa Jahazi hakuhitaji kupanda jukwaa moja na bendi yoyote ya Taarabu, jambo lililopelekea kufutwa kwa matangazo yote yaliyokuwa yakitangaza kuwepo kwa G5 Modern Taarabu ili uwepo yeye pekee, mdau mmoja alisikika akilalamikia jambo hilo akisema si vizuri kubaguana wakati wote ni bendi zinazopiga mziki mmoja!.

1 comments:

Anonymous said...

Inasikitisha sana kuskia msanii mkubwa km mzee Yusuf akifanya ubaguzi wa aina hiyo kwa kweli mm binapsi sioni mantiki ya yeye kukata kupanda jukwaa moja na bendi nyengine hukui akitambua wazi kua mashabiki wanataka burudani

Post a Comment