TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, September 8, 2013

MGENI KISODA AKANUSHA KUJIUNGA NA TWANGA PEPETA...

Mgeni Kisoda.
 Msaani aliejiengua toka Jahazi Modern Taarabu, Mgeni Kisoda leo hii amekanusha taarifa zilizozagaa mitaani kwamba amejiunga na Twanga Pepeta. 

Akizungumza na mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com Mgeni alisema kwamba anashangazwa na taarifa hizo za yeye kujiunga na bendi hiyo ya Twanga Pepeta ambapo yeye mwenyewe amesema si kweli na wala sina mpango, kama huo Muda ukifika wa mimi kwenda katika bendi yoyote basi itakuwa bayana wala haitokuwa kificho mimi ni msanii ninaefahamika kwahiyo ni lazima watajulishwa ni wapi nimeelekea. 
Ila kwa sasa nipo mgunda recoding nafanya vitu vyangu.

Na katika mtandao wa Facebook kawaambia mashabiki zake kwa status hii:-
"
Watu wangu mi mgeni kisoda sina bifu na jahazi sina bifu na mzee yusuph mi mi mwenyewe kwa mapenzi yangu nimeamuwa nibadilishe hali ya hewa nifanye ishu nyengine na tuombe mungu mtanisikia ivi karibuni bado nipo kama kawaida msikonde".

0 comments:

Post a Comment