TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, September 17, 2013

BREAKING NEWS - MSIBA: AHMED MGENI AFARIKI DUNIA LEO ZANZIBAR...

Marehemu, AHMED MGENI enzi za uhai wake.
Muimbaji Nyota na mashuhuli, mwenye uwezo mkubwa wa kuimba AHMED MGENI wa Zanzibar Njema amefariki dunia leo alfajiri huko visiwani unguja. 

Muimbaji huyo ambae amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu, alikuwa amelazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar. 

Akizungumza na mtandao huu dada wa marehemu aitwae LAISATY MGENI alithibitisha ni kweli Kaka yake amefariki dunia leo alfajiri visiwani humo.

Ahmed Mgeni enzi za uhai wake aliwahi kupitia bendi kadhaa za taarabu ila wimbo wake wa SITETEREKI ndio umempa sifa sana.

AHMED MGENI atazikwa leo Saa kumi jioni sehemu iitwayo Amani Fresh njia ya Ziwatue huko huko visiwani Zanzibar.

Taarabu Zetu tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na kipenzi chetu Ahmed Mgeni na mungu amlaze pema peponi, AMIN!!

DOWNLOAD NA SIKILIZA NYIMBO YA "SITETEREKI" YAKE AHMED MGENI..

2 comments:

Unknown said...

tulikupenda Mngu kakupenda zaidi, Allah ailaze roho yako mahali pema penye wema, akughufirie dhambi zako za siri na za dhahiri, akuepushe na adhabu ya kabri , pepo ya firdaus iwe makazi.

Anonymous said...

Innalillah wa inna ilayhi rajuuun

Post a Comment