TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, September 11, 2013

BREAKING NEWS: MGENI KISODA AJIUNGA SUPERSHINE MODERN TAARABU...

Mgeni Kisoda.
Aliekuwa mpiga kinanda namba moja wa bendi ya Jahazi Modern Taarabu, Mgeni Kisoda jana saa moja usiku amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Bendi ya Supershine Modern Taarabu. 

Mgeni kisoda ni mpiga kinanda wa siku nyingi aliyewahi kupigie Victoria Modern Taarabu, Dar es Salaam Modern Taarabu na nyingine nyingi kabla ya kujiunga na Jahazi Modern Taarabu. Baada ya kujiunga na Jahazi kisoda alikuwa mpiga kinanda namba moja katika Bendi hiyo kabla hajaondoka wiki moja iliyopita.

Kisoda alipoulizwa anajisikiaje kujiunga na Supershine na kwanini kachukua uamuzi mapema hivi!? Mwenyewe alisema: Ünajua unapokuwa mtu muhimu lazima watu wakusumbue, ni kipindi kifupi kweli na nimefuatwa na bendi nyingi zikitaka nikafanye kazi nazo lakini hatukuweza kufikia makubaliano, lakini Supershine wamefikia kiwango ninachokitaka na kwakuwa ni kati ya bendi nizipendazo, nimesaini nitakuwa pale sasa, nawakaribisha wapenzi wangu wote Supershine Modern Taarabu".

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi meneja wa bendi hiyo Kais Mussa Kais alisema hiyo ni moja ya mikakati yake madhubuti zaidi katika kuiinua bendi yake, "unajua kama nilivyosema katika mahojiano ya awali, nimekuja Supershine kuleta mabadiliko ya muziki wenyewe, mpaka wasanii ndani ya bendi, nilianza na Ndage Ndage na sasa ni Mgeni Kisoda. Nawaahidi wadau kazi nzuri inaendelea., kikubwa mtuunge mkono.

0 comments:

Post a Comment