TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, September 1, 2013

MGENI KISODA:- MIMI BADO NI MSANII WA JAHAZI MODERN TAARABU...

Mgeni Kisoda.
Mpiga kinanda wa Jahazi Modern Taarabu Mgeni Kisoda ameamua kuvunja ukimya na kusema kwamba yeye mpaka sasa bado ni msanii wa Jahazi Modern Taarabu na wala hajafukuzwa kama ambavyo taarifa zilizo zagaa Dar zinavyo vumishwa. 

Akizungumza na mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com Mgeni alisema: "Unajua kuna watu waliniona mimi katika show ya Twanga Pepeta wakaenda kumwambia Bosi wangu Mzee Yusuph kwamba eti mimi nimechukuliwa na bendi hiyo kwa sababu wameniona kule,  jambo ambalo sio kweli, mimi nilienda Twanga nilimpeleka mpiga kinanda mmoja baada ya jamaa kuniambia kwamba wanataka mpiga kinanda, hivyo mimi napenda kusema kuwa mpaka sasa bado ni msanii wa Jahazi Modern Taarabu na wapenzi wote wa bendi yetu mkija mtanikuta pale. Karibuni sana Jahazi...".

0 comments:

Post a Comment