TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, September 10, 2013

EAST AFRICAN MELODY KUFANYA SHOW JUMANNE NDANI YA MAX BAR ILALA...

 Bendi kongwe na yenye mashabiki wenye msimamo hapa jijini Dar es Salaam, East African Melody Siku leo Jumanne wanatarajia kufanya show katika ukumbi wa Max Bar Ilala. 

Akizungumza na mtandao huu katibu wa bendi hiyo Mr Abuu amesema kwamba, anawaomba wapenzi wa bendi hiyo kuja kwa wingi kwani wanatarajia kupiga nyimbo zao mpya kabisa ambazo zitawasisimua na kuwaburudisha zaidi. 

East African Melody ni bendi bora ya Taarabu nchini na ambayo siku za karibuni imeondokewa na viongozi wake wawili ambao ni Ramania na Haji Mohamedy, Mungu awalaze pema peponi amin!

0 comments:

Post a Comment