TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, July 23, 2013

5 STAR'S MODERN TAARABU, IDDI MOSI NDANI YA DAR LIVE MBAGALA...


Bendi ya 5 Stars Modern Taarab inataraji kutoa burudani ya nguvu kwa wakazi wa Mbagala kwenye ukumbi wa Dar live.

Akizungumza na mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com kiongozi wa bendi hiyo Jumanne Ulaya alisema siku ya Iddi mosi watapiga Dar live Mbagala, siku ya Iddi pili watapiga Rosh garden Mwandege na siku ya Iddi tatu tunatarajia kupiga Kibiti, tunawaomba wapenzi na mashabiki wetu waje kwa wingi kusikia nyimbo zetu mpya ambazo tumekuwa tukiziandaa wakati huu wa Ramadhan. 5 Stars wametambulisha nyimbo yao mpya jana kaimba Mwamvita.

Pia Jumaane Ulaya aliongeza kuwa, siku hiyo watawakumbushia wapenzi wao kwa kuimba nyimbo zao za nyuma zote ili kutoa burudani zaidi, anawaomba wapenzi wote wa 5Stars na Taarabu kwa ujumla kutokukosa show hiyo ya Idd Mosi.

0 comments:

Post a Comment