TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Saturday, July 13, 2013

DOMO LA UDAKU YAONGOZA KWA KUCHEZWA REDIONI MAY MPAKA JUNE...!


Nyimbo ya domo la udaku iliyoimbwa na msanii nguli, Gwiji wa Taarabu Jokha Kasimu toka Tanzania Motto Modern Taarab au "T MOTTO" ndio iliyoongoza kwa kuombwa na wapenzi katika redio mbalimbali na kuchezwa kwa sana kipindi chote cha mwezi MAY mpaka JUNE!.

Tathimini sahihi kabisa iliyofanywa na dawati la habari la taarabuzetu.blogspot.com ulithibitisha hilo baada ya kufanya uchunguzi kwenye vituo vya redio na wadau mbalimbali hapa nchini.

Domo la udaku ni wimbo unaobeba albamu mpya ya T Motto ambayo imebeba nyimbo takribani tano ambazo ni Domo la udaku yenyewe muimbaji Jokha Kasimu,
Behind the scene muimbaji Nyawana Fundikila,
Mwanamke hashuo muimbaji Shinuna Kasimu,
Wewe sio daktari wa mapenzi muimbaji Nassoro Hussein na
Ubaya una mwisho muimbaji Aisha Masanja.

Mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com unampongeza mkurugenzi wa T Motto Amin Salmin "Komandoo" na uongozi mzima wa Tanzania Motto kwa kutengeneza nyimbo bora na albam bora ya Domo la udaku!.