TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Monday, July 15, 2013

BAADA YA KIMYA KIREFU... ABDUL MISAMBANO AJA NA MBILI KALI....!


 Miaka ya nyuma wakati anatokea burundi alisumbua sana na wimbo wake wa "ASU", wimbo huu ulimpatia umaarufu mkubwa sana kwa mashabiki mbalimbali wa Taarabu hapa nchini. Huyu si mwingine ni Abdul Misambano ambae kwa sasa ni msanii wa TOT.

Misambano ameuambia mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com kwamba yupo mafichoni huko Dodoma akijifua kuandaa vibao viwili matata sana ambavyo ataviachia baada ya mfungo wa Ramadhani, alivitaja vibao hivyo kuwa ni "Si mie ni moyo" ambacho atakiimba katika style ya Rumba taarabu na cha pili ni "Ngoma chini style" ambacho nacho atakipiga kwa style ya sebene taarabu. Ameendelea kwa kusema kwamba nyimbo zote hizo mbili ataziimba nje ya bendi yake ya TOT.


Huu ni mpango wangu wa kukamilisha albamu yangu binafsi, nawaomba wapenzi na mashabiki wangu wakae mkao wa kupata burudani toka kwangu. Huyo ndio Abdul misambano au ukipenda mzee wa ASU!!.