TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, July 7, 2013

Bendi ya G5 Modern Taarabu kutambulishwa leo Tarehe 7/7/2013


Bendi mpya ya Taarabu jijini Dar es Salaam iitwayo G5 Modern Taarabu inatarajiwa kuzinduliwa leo siku ya Sabasaba katika Ukumbi wa Equator Grill - Mtoni kwa Azizi Ally, ikiwa na vibao vyake vipya kabisa.

Akizungumza na mtandao wa Taarabuzetu.blogspot.com Mkurugenzi wa bendi hiyo Hamisi Slim amesema ameanzisha bendi hiyo ili kuleta Ubora, Ushindani wa kikazi na Burudani zaidi.

Amewaomba wapenzi na Mashabiki wa Taarabu kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuwapa sapoti.