TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, July 10, 2013

HEE!! HAYA MAKUBWA....THABIT ABDUL MKONO WA MWANAUME MPAKA SASA HAKUMBUKI IDADI YA NYIMBO ALIZOSHIRIKI KUPIGA KINANDA....

Thabit Abdul akikung’uta kinanda kwa kidevu.
Mpiga kinanda namba moja kwa sasa katika tasnia ya Taarabu  nchini Thabit Abdul au "Mkono wa Mwanaume" kama anavyojulikana na wapenzi wake, ameuambia mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com kwamba mpaka sasa hakumbuki idadi kamili ya nyimbo alizoshiriki kupiga kinanda kwani ni nyingi mnoo!, "Unajua kaka mimi ni director ambae nimesaidia kuinua vipaji vya wasanii wachanga mbalimbali mpaka sasa wanafahamika", fikiria Bendi/mtu unamtoa akiwa hajulikani mpaka anakuwa maalufu, utakumbuka kweli!?.

Aliendelea kusema:- Nyumbani kwangu Kinondoni nina chuo cha mziki, pia nimepitia bendi nyingi sana na kote huko nimetengeneza nyimbo ambazo zimeendelea kutamba hadi leo,  kwahiyo sio rahisi kuweza kukumbuka idadi ya nyimbo nilizopiga maana ni nyingi.

Thabit Abdul kwa sasa ni msaani wa 5Stars ambae alinunuliwa kwa gharama kubwa sana akitokea Mashauzi Classic.