TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, July 14, 2013

BI MWANAHAWA ALLY, MSANII ANAE ONGOZA KUHAMA-HAMA BENDI... TATIZO NINI MAMAA...??

Mwanahawa Ally
 Masirahi... Masirahi... Masirahi, imekuwa kila msanii unaefanya nae mahojiano na anahama - hama bendi atakwambia hivyo, lakini baada ya muda anahama tena na kwenda bendi ingine kauli ni ile ile masirahi.

Huwa najiuliza huyo masirahi anaishi wapi ili ajitokeze na kutuliza roho za wasanii wetu?. Hapa ninao mfano wa Mama yetu Bi mwanahawa Ally au "Bi Kidude" kama anavyopenda kuitwa kwa sasa, kwa haraka haraka hizi ni baadhi tu ya bendi alizopitia:-
East African Melody,
Zanzibar Stars,
5Stars Modern Taarabu,
Jahazi Modern Taarabu,
T Motto Modern Taarabu,
Magereza Modern Taarabu ya Znz na nyingine nyingi.

 Mwenyewe ukimuuliza anasema maslahi, sasa tokea umeanza kutafuta masrahi hujapata? Huoni kama unawayumbisha mashabiki wako wasijue upo wapi?.

Mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com unakushauri kutulia na bendi moja ili iwe rahisi watu kujua ni wapi wakufuate na kupata burudani toka kwako mama!. Masirahi yatukuja tu...!!!