TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, July 17, 2013

JUMA MGUNDA "Jino Moja" WA JAHAZI MODERN TAARABU AFARIKI DUNIA MCHANA WA LEO....

Msanii wa zamani wa Jahazi Modern Taarabu aliyekuwa akipiga gitaa la Bass Juma Mgunda amefariki dunia mchana huu.

Juma Mgunda alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) kwa muda mrefu sasa, akizungumza na taarabuzetu.blogspot.com msanii mwenzake ambae ni rafiki yake wa karibu aitwae Mzaka Nundu amesema marehemu kipindi cha kati alikuwa vizuri tu baada ya kutumia vyema dawa za TB lakini ghafla khali ilibadilika jana na kukimbizwa Hospitali ya Temeke mpaka leo mchana akawa amefariki dunia.

Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwao Tandika katika stendi ya Gongolamboto.
Bwana ametoa na bwana ametwaa!!.