TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, July 23, 2013

BREAKING NEWS:- MSANII FATUMA CHUKI WA SEGERE AFARIKI DUNIA!!.


Kundi La Segere

Muimbaji wa kikundi cha segere Fatuma Chuki amefariki dunia mchana wa leo Tarehe 23 Julai 2013 katika Hospitali ya Muhimbili.

Kwa mujibu wa msanii mwenzie ambae alikuwa nae karibu sana Bwana Ng'onda wa East African Melody ameuambie mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifua kwa muda mrefu mpaka leo umauti ulipomfika!.

Wakati wa uhai wake marehemu aliwahi kufanya kazi bendi mbalimbali lakini alikuja kujulikana zaidi pale alipotoa wimbo wa segere namba 2 ambamo ndani yake kulikuwa na maneno yakufurahisha mno.
Msiba umewekwa kwao Mwananyamala B tayari kwa mazishi.

0 comments:

Post a Comment