TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, July 7, 2013

Funga Kazi Modern Taarabu yaja na Nne kali!!

Funga Kazi Modern Taarabu.
Funga Kazi Modern Taarabu ni bendi inayokuja kwa kasi sana katika tasnia ya Taarabu nchini Tanzania, imefanikiwa kurekodi vibao vyake vipya Vinne.

Akizungumza na mtandao wa Taarabuzetu.blogspot.com Mkurugenzi wa bendi hiyo Kapteni Temba alizitaja nyimbo hizo na waimbaji wake katika kundi hilo ni:-
1. Inzi wa Kijani (Ashura Machupa)
2. Muungwana haumbuki (Wahida Dadi)
3. Msitake tuvurugane (Kapteni Temba) na
4. Si bure unaradhi ya Mume (Salma Mikausho)

Mkurugenzi wa Funga Kazi Modern Taarabu Kapteni Temba amesema katika kipindi cha Ramadhani ataachia nyimbo mbili ambazo alizitaja ni:-
1. Inzi wa Kijani (Ashura Machupa) na
2. Muungwana Haumbuki (Wahida Dadi)

Wakati huohuo Funga kazi Modern Taarabu imepata Meneja mpya aitwaye Muhsin Masoud mtoto wa Mwanza.