TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, July 24, 2013

FATUMA CHUKI WA SEGERE AZIKWA BAGAMOYO LEO SAA 5 ASUBUHI...

 Msanii wa kundi la Segere Fatuma Chuki ambae amefariki jana katika Hospitali ya Muhimbili amezikwa leo saa 5 nyumbani kwao katika chimbuko la wazazi wake Bagamoyo. 

Mwili wa marehemu ulipelekwa jana ile ile Mwananyamala lakini baada ya kusomewa Dua mwili ulipakiwa katika gari na msafara wa kuelekea Bagamoyo ulianza jana ile ile, ambapo leo uliweza kuzikwa muda mchache uliopita. 

Akizungumza na mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com ndugu wa marehemu Salehe Madebe aliwashukuru ndugu jamaa na marafiki wote walioshiriki katika mazishi hayo ya mpendwa wao Fatuma Chuki na wote walioshiriki kwa namna yoyote ile.

0 comments:

Post a Comment